Show simple item record

dc.contributor.authorAlexander, Andy, S.J.
dc.contributor.authorWaldron, Maureen McCann
dc.date.accessioned2018-02-08T22:36:44Z
dc.date.available2018-02-08T22:36:44Z
dc.date.issued2000-01-01
dc.identifier.urihttp://hdl.handle.net/10504/116837
dc.description.abstractJUMA LA KUMI NA MOJA|Mwaliko wa Kupenda — Mwitikio Wetu|Mwongozo: Kufanya Majitoleo ya Nafsi Kikamilifu|Katika Juma hili tuitikie kwa moyo mwaliko wa mapendo tulioupata. Kupitia katika zoezi la juma lililopita, tumeweza kujua kuwa sifa ya mwitikio wetu inategemea kina cha upendo wetu kwa yule atualikaye. Pale mpendwa wetu anapotuuliza kuhusu mwitikio wetu kwa mwaliko wake, jibu ni “Ndiyo”. Hata pale tunapojua kuwa mwitikio huu unaendana na gharama binafsi kubwa sana, bado mwitikio wetu haubadiliki kwa kuwa tunajua upendo daima unatuweka katika ukaribu na umoja wa wapendanao—nasi tunataka daima kuwa na yule tumpendaye.|Kwa mioyo yetu, juma hili tutakuwa tukiitikia mwaliko wa Yesu Kristu. Tunaweza kwa muda mfupi kufanya marudio ya mwongozo wa zoezi la juma lililopita ili kujikumbusha mwito huu na kuamsha hisia za rohoni tulizopata. Tuliguswa sana na mwaliko wa kuungana naye katika mradi wa kuwaleta wengi katika kuwakaribisha wengi katika utawala wa Mungu. Tukiangalia kwa makini, tutaona kuwa mwito huu unatofautiana kidogo kutoka mtu mmoja hadi mwingine kwa kuwa tuna vipaji, historia na malezi tofauti. Mioyoni, tumezawadiwa neema tofauti baina ya mtu mmoja na mwingine. Hali ya maisha tuliyopitia; namna mbalimbali za kheri na shari, furaha na huzuni, mahangaiko na starehe; vimetujengea kila mmoja namna tofauti na ya kipekee ya kuhurumia na kuwa na wengine katika magumu yanayowasibu. Kila mmoja wetu anapata mwaliko kwa namna yake ya pekee, kulingana na umri na uwezo tuliojaliwa hasa wa ushawishi kwa wengine. Hivi basi tunapenda kusikia mwaliko wa Kristu ukielekezwa kwetu binafsi, kama vile tukialikwa kwa kutajwa majina na yule atupendaye. Hata hivyo, kwetu sote, kuna usawa katika mwaliko na nafasi tunayopewa ya kuuitia. Bila shaka mwitikio wetu ni “Ndiyo”. Hakuna furaha ya kweli maishani ambayo haihusishi kumfuasa Yesu Kristu. Swali la juma hili ni kina au upevu wa mwitikio wetu—jinsi ambavyo tunaweza kuuitikia kikamilifu mwito wa Kristu. Hatujui kwa uhakika bayana “Ndiyo” yetu mwaka huu itakuwa namna ipi na itajumuisha yapi. Kadhalika hatuweze kuwa na habari kamili za “Ndiyo” yetu mwaka ujayo, au miaka kumi kutoka leo.|Maandiko Matakatifu|Isaya 6:1-8|Zaburi 116|Luka 10:1-9; 17-21|Yohana 21:15-19en_US
dc.language.isoen_USen_US
dc.publisherCreighton University, Online Ministriesen_US
dc.subject.otherKiswahili Language
dc.titleWeek 11 Guide: Juma 11en_US
dc.typeText
dc.publisher.locationOmaha, Nebraska, United States
dc.description.noteActual date of publication unknown. The date in dc.date.issued is arbitrary and used because a date is required for indexing
dc.relation.nexthttp://hdl.handle.net/10504/116838
dc.relation.previoushttp://hdl.handle.net/10504/116835


Files in this item

Thumbnail
Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record