Week 16 Guide: Juma 16
Browse: Previous Reflection * Next Reflection
Retreat Guide: Opening Text and Content
To see the original html pages, PDFs and audio files, click the file links on the left.JUMA LA KUMI NA SITAMaisha Nje ya Hadhara kwa Miaka ThelathiniMwongozo: Mwana wa SeremalaMojawapo ya ukweli wa kushangaza sana kumhusu Yesu Kristu ni kuwa tunajua kidogo sana kuhusu maisha yake katika miaka thelathini ya mwanzo wa maisha yake. Tunajua alipoanza kazi yake hadharani, wali walimjua yeye na ndugu zake walishangazwa sana. Kwa dharau wengine walitoa mashambulio yao dhidi yake wakisemezana: “huyu siye yule mwana wa seremala?”Juma hili la mafungo linatupa muda wa kumjua Yesu anayekua katika ubinadamu wake (anayeongezeka umri). Kwa kuwa kuna Maandiko machache sana ya kurejea kuhusu maisha yake kati ya kuzaliwa kwake na kubatizwa kwake, tutatumia ubunifu wetu kujazia sehemu zile ambazo hatuambiwi mengi na maandiko—ila tunajua kweli mbalimbali za historia ya wakati huo, kazi ya baba yake, imani na tamaduni za watu wake, n.k. Zaidi, kama tukiifikiria hali ya utu-uzima ambayo Yesu alifikia, tunaweza pia kutafakari jinsi utoto wake ulivyokuwa, alikuwa mtoto wa namna gani, mambo gani alipambana nayo katika maisha na fikara, ni maamuzi gani hasa alifanya, n.k. Kwa kutumia kile tunachojua kuhusu maendeleo ya watoto hadi kufikia ujana, halafu kufikia utu uzima, tunaweza kufanya ubunifu mzuri kuhusu mambo kadhaa ya kibinadamu ambayo sharti Yesu aliyakabili. Tukisali namna hii tuingie katika zoezi la kumjua kwa undani zaidi, ili kwamba tuweze kumpenda zaidi na kufikia shauku yetu ya ndani kabisa ya kuwa naye katika utume wake aliopewa na Mungu Baba.Maandiko MatakatifuLuka 2:22-38Luka 2:39-40Luka 2:41-52Waebrania 1:1-2